Mpanda FM

Zaidi ya wanafunzi 40 wa chuo cha Kilitech watunukiwa vyeti

19 December 2025, 6:49 pm

Wahitimu wa chuo cha ufundi Kilitech. Picha na Anna Mhina

“Kwa suala la upungufu wa komputa niachieni mimi”

Na Anna Mhina

Chuo cha ufundi Kilitech VTC mkoani Katavi kimefanya mahafali yake ya nne (4)  December 18, 2025 ambapo zaidi ya wahitimu arobaini (40) wametunukiwa vyeti na stashahada katika fani mbalimbali za ufundi.

Akitoa hotuba yake mgeni rasmi ambaye ni meneja biashara wa CRDB Bank Amos Twaru mbali na kutatua changamoto zinazokikabili chuo hicho pia amewataka wahitimu kujiunga na taasisi za kifedha ili kuweza kujikwamua kiuchumi.

Sauti ya mgeni rasmi

Awali akisoma risala kwa mgeni rasmi  mkuu wa chuo cha ufundi Kilitech VTC Baraka Ledson ameeleza changamoto zinazowakabili ikiwa ni pamoja na ufinyu wa eneo la chuo sambamba na upungufu wa vifaa vya kufundishia kama vile computer.

Sauti ya mkuu wa cguo

Kwa upande wao baadhi ya wahitimu wa chuo hicho wameeleza furaha yao na kuahidi kuwa mabalozi wazuri wa chuo kwa kutumia taaluma zao kwa uadilifu na bidii.

Sauti za wahitimu

Mahafali hayo yamehitimishwa kwa utoaji wa tuzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri kitaaluma, nidhamu, michezo ,usafi, uvumilivu pamoja na tuzo ya mtunzaji bora wa mazingira.