Mpanda FM

Tanzania kujadili utekelezaji makubaliano COP30

16 December 2025, 10:01 pm

Picha na mtandao

“hatuhitaji tena kubaki kwenye ngazi ya ahadi tunataka mifumo madhubuti”

Na Restuta Nyondo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuongoza kikao maalum cha wadau wa mazingira na maendeleo kujadili mwelekeo wa nchi katika utekelezaji wa maamuzi na makubaliano baada ya COP30.

Kikao hicho kimeelezwa kuwa cha kimkakati katika kuunganisha ahadi za kimataifa na vipaumbele vya taifa, hususani katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na kuchochea maendeleo endelevu.

Akizungumza na waandishi wa habari zinazohusu masuala ya manadiliko ya tabia nchi na mazingira kilichoandaliwa na Tanzania Media Foundation Mshauri wa Rais kuhusu Masuala ya Mazingira na Mwenyekiti wa Kundi la Majadiliano la Afrika (AGN), Dar es Salaam, Dkt. Richard Muyungi, amesema kikao hicho ni fursa ya kutafsiri maamuzi ya COP30 kuwa hatua za utekelezaji zinazoonekana kwa wananchi.

Sauti ya dkt.Richard Muyungi

Amesema Tanzania inapaswa kuimarisha mifumo ya uwajibikaji ili kuhakikisha ahadi za kimataifa zinageuka kuwa mipango yenye tija kuanzia katika ngazi za serikali za mitaa na kugusa mikoa iliyopo pembezoni kama vile Katavi kupitia mifuko mbalimbali iliyoanzishwa ikiwemo mfuko wa hasara na uharibifu.

sauti ya dkt.Muyungi

Kikao hicho kinatarajiwa kufanyika december 17 ambacho kitalenga katika kutoa mwelekeo wa Tanzania kuhusu vipaumbele vya utekelezaji wa maamuzi ya COP30, mgawanyo wa majukumu kwa taasisi husika na mfumo wa kufuatilia matokeo.