Mpanda FM
Mpanda FM
11 December 2025, 12:46 pm

“Watoto wa sasa hivi hawawasikilizi wazazi wao”
Na Janeth Kaombwe
Katika kuadhimisha siku ya haki na maadili kitaifa inayofanyika tarehe 10 mwezi wa 12 kila mwaka, vijana wamehimizwa kuendelea kufuata maadili ya kitanzania kwani kumekuwa na mmomonyoko wa maadili kwa vijana Tanzania.
Wakizungumza na Mpanda radio FM baadhi ya wazee mkoani katavi wamesema kuwa maadili ya sasa ni tofauti na ya zamani kwani vijana wengi hawafuati maelekezo wanayopewa na wazazi wao wala kujituma katika shughuli mbalimbali za kiuchumi.
Kwa upande wa baadhi ya vijana wa manispaa ya Mpanda wamekiri kuwepo kwa mmomonyoko wa maadili unaosababishwa na vijana wengi kukosa heshima na mwitikio mzuri kutoka kwa wazazi wanapowatuma kufanya vitu mbalimbali .