Mpanda FM
Mpanda FM
11 December 2025, 12:19 pm

Picha ya shule ya msingi Mpanda. Picha na Anna Mhina
“Mzazi anapokuja kumuandikisha mtoto ni marufuku kumwambia hatuna nafasi”
Na Anna Mhina
Wazazi na walezi wilayani Mpanda wametakiwa kujitokeza mapema katika kuwaandikisha watoto shule hususani darasa la kwanza na awali ili kuweza kuepuka usumbufu unaojitokeza kipindi cha mwezi January.
Akizungumza na Mpanda radio FM mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph amesema watoto wenye umri wa miaka mitano wanapaswa kwenda kuandikishwa darasa la awali huku wenye umri wa miaka sita wakaandikishwe darasa la kwanza na kuwasihi walimu kutokuweka ukomo wa kuwapokea wanafunzi kwa kisingizio cha kusema darasa limejaa.
Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa shule ya msingi Mpanda Magreth Alphoce Sumia ambaye ni mwalimu katika shule hiyo amesema mpaka sasa wanafunzi walioandikishwa darasa la kwanza ni 22 huku darasa la awali wakiwa 13 na kueleza changamoto wanayoipata pindi wazazi na walezi wanapochelewa kuwaandikisha watoto ikiwemo kushindwa kuanza kufundisha.
Kwa upande wao baadhi ya wazazi na walezi wameeleza namna walivyojiandaa kuhakikisha watoto wao wananza shule msimu wa mwaka 2026 huku wengine wakieleza sababu za kuchelewa kuwaandikisha ikiwemo kutoa kipaombele sherehe za sikukuu.