Mpanda FM
Mpanda FM
8 December 2025, 4:36 pm

“Inanipa uhuru wa kupumua na kuwa na afya njema”
Na John Benjamin
Baadhi ya vijana wilaya Mpanda mkoani Katavi wametaja matumizi ya njia za uzazi wa mpango yana mchango katika kuboresha ustawi wa jamii na mahusiano ya kifamilia.
Wakizungumza na Mpanda Redio kwa nyakati tofauti wamesema kuwa njia hizo husaidia kupunguza ongezeko la watoto wanaoishi mtaani na kuchochea maendeleo ya kiuchumi kwa familia na jamii kwa ujumla na wamesisitiza kuwa elimu ya uzazi wa mpango bado inahitajika kwa kiwango kikubwa ili jamii iweze kufahamu faida zake na kuondokana na dhana potofu zinazohusishwa na matumizi ya njia hizo.
Kwa upande wake mratibu wa afya mama na mtoto mkoa wa Katavi Elida Machungwa amesema njia za kisasa uzazi wa mpango zinamanufaa makubwa katika afya ya uzazi ambapo ameleeza kuwa matumizi sahihi ya njia hizo humsaidia mama kupata muda wa kutosha wa kupumzika baada ya kujifungua na kushiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji mali na hupunguza vifo vya mama na mtoto
Aidha Machungwa ametoa wito kwa wazazi na walezi kuendelea kujitokeza katika vituo vya afya kupata ushauri sahihi kuhusu njia mbalimbali za uzazi wa mpango ili kujenga familia imara na kuchochea maendeleo endelevu katika mkoa wa Katavi na nchi kwa ujumla.