Mpanda FM
Mpanda FM
8 December 2025, 3:03 pm

“Kukamilisha malengo kwanza unatakiwa uwe na msimamo”
Na Leah Kamala
Baadhi ya wananchi wa manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wametoa maoni yao kuhusiana na umuhimu wakujiwekea malengo ili kuboresha maisha yao binafsi.
Wakizungumza na Mpanda radio FM wananchi hao wamesema kuwa kujiwekea malengo ni hatua muhimu inayoweza kumsaidia mtu kupiga hatua katika maisha na kumuwezesha kufanikisha jambo fulani.
Nae Afisa maendeleo mkoa wa Katavi Anna Shumbi amesema kuwa kuweka malengo kunawasaidia vijana wengi kujiepusha na matumizi mabaya ya fedha hivyo amewasihi vijana kujiwekea malengo.
Ameongeza kuwa kutojiwekea malengo kunawafanya wananchi kushindwa kupanga matumizi yao na kukosa mwelekeo wa kiuchumi.