Mpanda FM
Mpanda FM
6 December 2025, 12:32 pm

“Sisi kama viongozi wa dini tutashirikiana na wananchi katika kudumisha amani”
Na Restuta Nyondo
Viongozi wa dini mkoani Katavi wametoa tamko la amani na kuhamasisha utulivu na ushirikiano kwa wananchi huku wakisema ni wajibu wa kila mtu kulinda amani na usalama wa nchi.
Tamko hilo limesomwa na padri James Katagwa mwenyekiti wa jumuia ya maridhiano na Amani wilaya ya Mpanda amesema kuwa wao kama viongozi wa dini wapo tayari kwenda kuitangaza imani na kushirikiana na waumini katika kulinda amani.
Awali akifungua kikao hicho mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko amewaomba viongozi hao katika mafundisho yao kuendelea kuwaasa wazazi na walezi juu ya malezi yenye maadili kwa vijana wao.
Aidha amesema kuwa viongozi wa dini ni tanuru la amani kwa wananchi, na kuwataka kuendelea kutumia njia ya mazungumzo na ushauri ili kuleta maendeleo.