Mpanda FM

Wananchi Katavi hatarini kupata magonjwa ya mlipuko

4 December 2025, 12:13 pm

Picha ya takataka zilizotelekezwa. Picha na Samwel Mbugi

“Serikali naishauri iongeze magari yanayobeba taka”

Na Samwel Mbugi

Baadhi ya wananchi wa manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi wameiomba serikali kuendelea kutoa elimu ya usafi wa mazingira kipindi hiki cha mvua zilizoanza kunyesha ili kujiepusha na magonjwa ya mlipuko kama vile kipindupindu.

Wakizungumza na Mpanda radio wamesema kipindi cha mvua huwa kuna magonjwa ya mlipuko ambayo huwa yanajitokeza, hivyo serikali iendelee kutoa elimu kupitia kwa viongozi mbalimbali wa maeneo husika ili wananchi wajue namna ya kuchukua tahadhari ya magonjwa hayo.

Sauti ya wananchi

Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa, kaimu katibu tawala mkoa wa katavi Florence Chrisant amethibitisha uwepo wa mazingira machafu ambapo amewataka viongozi wa ngazi husika na watendaji wa kata kuhakikisha wanasimamia mazingira yanakuwa masafi kila wakati hususani kipindi hiki cha msimu wa Mvua ambazo zimeanza kunyesha.

Sauti ya Chrisant

Sambamba na hilo Chrisant amewataka watendaji wa kata na maafisa maendeleo kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi wa kuzitatua.