Mpanda FM

Viongozi wa Kidakio cha Mto Katuma walia na wafugaji

4 December 2025, 9:03 am

Viongozi wa kidakio cha mto Katuma na wafugaji katika picha ya pamoja. Picha na Restuta Nyondo

“Wafugaji hawaelewi ukimwambia leo kesho anarudia tena”

Na Restuta Nyondo

Ongezeko la mifugo katika eneo la Kidakio cha Mto Katuma imetajwa kuwa chanzo cha uharibifu wa vyanzo vya maji mkoani Katavi.

Felista Madeleke mjumbe wa kamati mto Katuma amesema kuwa bado baadhi ya wafugaji hawana elimu ya kutosha kuhusu uhifadhi wa vyanzo vya maji hivyo wamekua wakihamia na mifugo mingi bila kufuatwa kwa utaratibu na kuchangia uharibifu mkubwa katika maeneo hayo.

Sauti ya Madeleke

Kwa upande wake katibu wa wafugaji wilaya ya Tanganyika amesema kuwa changamoto hiyo inatokana na serikali za vijiji kuvamia maeneo  yaliyotengwa kwaajili ya malisho na kunyweshea mifugo.

Sauti ya katibu wa wafugaji

Thadeus Ndeseiyo ni afisa uhusiano wa bonde la maji ziwa Rukwa amesema kuwa wamekua wakichukua hatua mbalimbali za kisheria katika kudhibiti changamoto hiyo lakini bado uvamizi huo unaathiri uwezo wa uzalishaji maji katika vyanzo hivyo.

Sauti ya afisa uhusiano

Kidakio cha mto Katuma ni miongoni mwa vidakio 7 katika bonde la ziwa Rukwa ni miongoni mwa kidakio muhimu katika kupeleka maji katika hifadhi ya taifa Mkomazi  na shughuli za kilimo,ufugaji na matumizi ya nyumbani kwa wakazi wa mkoa wa Katavi.