Mpanda FM

Makundi hatarishi yakwamisha maendeleo ya vijana Katavi

3 December 2025, 3:56 pm

Afisa maendeleo ya jamii Katavi Anna Shumbi. Picha na Anna Mhina

“Wawe makini katika kuangalia tabia na marafiki walionao”

Na Anna Mhina

Vijana mkoani Katavi wametakiwa kuwa makini katika kuchagua marafiki wa kuambatana nao ili kuweza kuepuka kujiunga na makundi mabaya yatakayohatarisha maisha yao.

Akizungumza na Mpanda radio FM afisa maendeleo ya jamii mkoa wa Katavi Anna Shumbi amesema kijana anapaswa kuwa makini katika kuchagua rafiki wa kuambatana nae ili kuweza kujenga maisha yake.

Sauti ya Anna Shumbi

Katika hatua nyingine Shumbi ameeleza madhara yatakayompata kijana endapo atajiunga na makundi mabaya ikiwemo kushindwa kufikia ndoto zake pamoja na kuhatarisha usalama wake binafsi kwa kuishia jela.

Sauti ya Anna Shumbi

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa Mpanda hotel wameeleza sababu zinazopelekea vijana kujiunga na makundi mabaya ikiwa ni pamoja na baadhi ya malezi ya wazazi sambamba na ukosefu wa ajira.

Sauti za wananchi

Hata hivyo serikali imejipanga kushughulikia changamoto zinazowakumba vijana kwa kuunda wizara maalum itakayoshughulika na changamoto zao ili waweze kujiepusha na makundi mabaya.