Mpanda FM
Mpanda FM
27 November 2025, 11:58 am

“Tunaihamasisha jamii itunze vyanzo vya maji kwa sababu ni muhimu”
Na Leah Kamala
Baadhi ya wananchi wa manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameeleza madhara katika mazingira endapo vyanzo vya maji vitaharibiwa.
Wakizungumza na Mpanda radio FM wananchi hao wamesema kuwa madhara hayo yanaweza kusababisha kupungua kwa uzalishaji wa umeme pamoja na kuongezeka kwa magonjwa hivyo wameiomba serikali iendelee kutoa elimu ili kuepukana na madhara hayo.
Naye Afisa Mazingira Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi Zaituni Rashid amewaelezea wananchi juu ya umuhimu wa kuhifadhi vyanzo vya maji ili kuhakikisha upatikanaji wa maji safi pamoja na kudumisha mazingira na ustawi wa viumbe hai
Ni muhimu kwa jamii, serikali na taasisi mbalimbali kushirikiana kulinda vyanzo vya maji kwa ajili ya uzalishaji wa chakula na kuhifadhi mazingira