Mpanda FM
Mpanda FM
27 November 2025, 9:26 am

Na Anna Mhina
Baadhi ya wananchi wa manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameiomba serikali kutoa elimu ya masuala ya uzazi wa mpango ili waweze kuepukana na mimba zisizotarajiwa.
Wakizungumza na Mpanda radio FM wananchi hao wamesema kuwa wanapewa dawa za uzazi wa mpango bila kupewa elimu ya kutosha hali inayopelekea kupata maudhi huku wanaume wakidai kuwa elimu hii inawafikia wanawake pekee.
Kwa upande wake mtaalam wa afya na kaimu mratibu wa mama na mtoto mkoa wa Katavi Mercy Hezekia ameeleza hatua zitakazosaidia vijana kuepuka mimba zisizotarajiwa ikiwemo kutoa elimu ya afya ya uzazi wa mpango pamoja na kuelimisha kuhusu njia za uzazi wa mpango.
Hata hivyo elimu inahitajika zaidi katika kufuta dhana potofu kuhusu uzazi wa mpango huku wanaume wahamasishwe kushiriki katika maamuzi ya uzazi wa mpango ili kupunguza mzigo wa kumuachia mwanamke pekee.