Mpanda FM

Wafanyabiashara walia na miundombinu ya soko la Mpanda hotel

26 November 2025, 10:51 am

Katibu wa soko la Mpanda hotel Haji Mponda. Picha na Samwel Mbugi

“Mvua zinazoendelea kunyesha zinaleta madhara makububwa “

Na Samwel Mbugi

Wafanyabiashara wa soko la Mpanda hotel wameiomba serikali kushughulikia changamoto ya mifereji ya kupitishia maji hususani kipindi hiki cha mvua zilizoanza kunyesha ili isije kuleta madhara ya magojwa ya mlipuko.

Wameyasema hayo wakizungumza na Mpanda radio FM kuwa kipindi hiki ambacho mvua zimeanza kunyesha kumejitokeza madhara ya kujaa kwa maji katika soko hilo na kusababisha kukosa wateja wa bidhaa zao ambazo zinakuwa zimeshalowa.

Sauti za wafanyabiashara

Katibu wa soko la Mpanda hotel Haji Mponda amesema kutokana na changamoto hiyo, kupitia kwa afisa biashara mkoa wa Katavi alifika eneo hilo na kuahidi kulifanyia kazi kwa kwenda kuonana na TARURA ili wafanye marekebisho ya mfereji uliopo upande wa soko hilo.

Sauti ya katibu wa soko