Mpanda FM
Mpanda FM
22 November 2025, 10:31 am

Waziri Mbarawa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa bandari hiyo. Picha na Samwel Mbugi
“Sasa tunajenga meli nne kwa mpigo”
Na Samwel Mbugi
Waziri wa uchukuzi Makame Mbarawa amelizishwa na utengenezaji wa meli nne zinazotengenezwa bandari ya Karema mkoani Katavi.
Akizungumza Mara baada ya ukaguzi amesema kukamilika kwa meli hizo kutochochea uchumi mkoa wa Katavi na kila meli itakuwa na uwezo wa kubeba tani elfu mbili.
Pia ametoa wito kwa wananchi watakaopata ajila ya kufanya kazi katika bandari hiyo kuwa waaminifu kwa kusimamia usalama vya vyombo na mizigo katika bandari hiyo.
Kwa upande wake Edward Mabula meneja wa Bandari ziwa Tanganyika amesema kati ya meli hizo nne moja imekamilika kwa asilimia 90% na ipo tayari kwa majaribio.
Hata hivyo mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph aliyemwakilisha mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko amesema kukamilika kwa meli hizo kunaenda kuufungua mkoa wa Katavi kiuchumi.