Mpanda FM

Wanaume jihusisheni na njia za kisasa za uzazi wa mpango

19 November 2025, 10:55 am

Mratibu wa mama na mtoto mkoa wa Katavi Elida Machungwa. Picha na Anna Mhina

“Njia za uzazi wa mpango ni muhimu kwa jinsia zote kuzifuata”

Na John Benjamin

Baadhi ya vijana kutoka halmashauri ya manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wametoa maoni tofauti kuhusu mlengwa wa kutumia njia za kisasa za uzazi wa mpango.

Wakizungumza na Mpanda redio FM kwa nyakati tofauti wamesema kuwa jamii imekuwa ikimtazama mwanamke kama mtu anayepaswa kubeba jukumu hilo ambapo kupitia mtazamo huo vijana hao wamesema kuwa jukumu hilo ni la kila mmoja kuwajibika kupanga uzazi kwa sababu ni sehemu ya uhusiano na wanahusika katika kupanga maisha ya familia.

Sauti za wananchi

Kwa upande wake mratibu wa mama na mtoto mkoa wa Katavi Elida Machungwa amesisitiza kuwa uzazi wa mpango si wajibu wa jinsia moja bali ni jukumu la mwanaume na mwanamke akibainisha kuwa njia nyingi za uzazi wa mpango zinahitaji maamuzi ya pamoja na ushirikiano wa karibu ili ziweze kufanya kazi kwa ufanisi.

Sauti ya mratibu

Serikali nchini kupitia wizara ya afya imeendelea kutoa elimu kwa jamii kufahamu kupanga uzazi ni wajibu wa kila mmoja na ni msingi wa kutengeneza kizazi chenye afya na uelewa.