Mpanda FM
Mpanda FM
18 November 2025, 6:59 pm

Afisa ustawi manispaa ya mpanda Anyulumye Longo. Picha na Leah Kamala
“Vikao vinasaidia kusuluhisha migogoro”
Na Leah Kamala
Baadhi ya wananchi wa manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameitaka jamii kujenga mazoea ya kukaa na kuzungumza katika vikao vya familia.
Wakizungumza na mpanda radio FM wananchi hao wameeleza kuwa vikao vya familia ni msingi muhimu wa kudumisha umoja, kuelekezana, pamoja na kutatua changamoto zinazoikabili familia ili kuimarisha mahusiano ya kifamilia.
Nae afisa ustawi manispaa ya mpanda mkoani Katavi, Anyulumye Longo amesema kuwa vikao vya familia ni nguzo kuu za ustawi wa jamii kwani husaidia kujenga maadili na kutatua migogoro iliyopo kwenye familia.
Longo ameongeza kuwa endapo familia zitashindwa kufanya vikao huweza kupelekea mipango mingi ya familia kushindwa kutekelezeka.