Mpanda FM
Mpanda FM
17 November 2025, 12:59 pm

“Lengo ni kutoa fursa kwa ajili kuongeza uzalishaji wa mafuta ya alizeti”
Na Restuta Nyondo
Kuanzishwa kwa jukwaa la wadau wa zao la alizeti mkoani Katavi kunatajwa kama mwanzo wa utatuzi wa uhakika kwa baadhi ya changamoto zinazokabili kilimo cha zao hilo.
Akizungumza na Mpanda Radio Fm mwenyekiti wa chama cha wasindika mafuta ya alizeti Tanzania (TASUPA) na mratibu wa majukwaa ya wadau wa zao la alizeti bw. Ringo Iringo amesema kuwa majukwaa hayo ni daraja kati ya wadau wa zao hilo na serikali kutambua fursa na changamoto ya uzalishaji wa zao hilo katika kuongeza mnyonyoro wa thamani.
Jukwaa hilo linajumisha wakulima, wachakataji, wasindikaji ,wauzaji wa pembejeo,serikali na wadau mbalimbali wanaeleza kuwa jukwaa hilo litakwenda kuwasaidia katika kupata elimu zaidi ya kilimo hicho na namna ya kupata masoko ya zao hilo.
Frank Kaminyoge ni meneja miradi mkoa wa Katavi kutoka shirika la Rikolto amesema kuwa kupitia mradi wa kuongeza mnyonyoro wa thamani katika zao la alizeti amesema kuwa zao hilo bado linakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa teknolojia bora za uzalishaji na uchakataji.
Mpaka sasa Tanzania ina jumla ya majukwaa ya wadau wa zao la alizeti 12 katika mikoa 12 ya Tanzania.