Mpanda FM

Athari za mabadiliko ya tabianchi mwiba kwa zao la alizeti Katavi

17 November 2025, 10:20 am

Shamba lilioandaliwa kwaajili ya kupanda alizeti. Picha na Restuta Nyondo

Na Restuta Nyondo

Karibu kusikiliza makala fupi inayozungumzia athari za mabadiliko ya tabia nchi kwa zao la alizeti mkoani Katavi wakati mkutano wa 30 wa nchi wanachama wa mkataba wa umoja wa mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi (COP30) ukiwa unaendelea katika jiji la Belém do Pará, nchini Brazil.

Wakulima,wasindikaji na wadau wa zao hilo wametaka fedha zinazotolewa kwaajili ya hasara na uharibifu zijikite kuboresha teknolojia bora za kisasa ili kuwa kuwa na kilimo endelevu na chenye tija.