Mpanda FM

Matarajio ya wananchi Katavi kuelekea mkutano wa COP30

8 November 2025, 2:05 pm

Picha ikionesha hali ilivyo kwasasa katika ukingo wa eneo la mto Misunkumilo. Picha na Restuta Nyondo

“Mkutano huu ni muhimu kwa Tanzania kwani tutaweza kulinda misitu ya asili”

Na Restuta Nyondo

Jamhuri ya muungano wa Tanzania imethibitisha kushiriki katika Mkutano wa 30 wa nchi wanachama wa mkataba wa umoja wa mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi (COP30) unaotarajiwa kuanza Novemba 10-21,2025 kwenye jiji la Belém do Pará, nchini Brazil.

Kutokana na umuhimu wa COP30 ambalo ni jukwaa rasmi la kimataifa kwa ajili ya kujadili na kutafuta ufadhili wa fedha za kukabiliana na madhara ya mabadiliko tabianchi na kufikia makubaliano ya kimataifa yanayoathiri sera za kitaifa za utekelezaji wake kama vile mkataba wa Kyoto na Paris, Tanzania inayo nafasi ya kutafuta fedha za kukabiliana na changamoto mbali mbali ikiwemo mafuriko.

Mpanda radio FM  imefanya mazungumzo na afisa mazingira kutoka halmashauri ya manispaa ya  Mpanda Bi. Zaituni Rashid ambapo amesema kuwa mkutano huo ni muhimu nchini Tanzania kwaajili ya kupata misaada ya kifedha kama wahanga wa mabadiliko ya tabianchi.

sauti ya afisa mazingira manispaa ya Mpanda

Aidha amesema kuwa anatarajia matokeo ya mkutano huo kuugusa mkoa wa Katavi hasa katika uboreshaji wa sera ambazo zitalinda makubaliano ya masuala ya mazingira.

sauti ya afisa mazingira manispaa ya Mpanda

Mkutano wa mwaka huu ni mwendelezo wa mikutano hiyo inayofanyika kila mwaka tangu mwaka 1995 na msingi wake ni mkutano wa mazingira wa dunia uliofanyika Brazili mwaka 1992 ambao uliridhia kuanzishwa kwa COP ambayo ni kifupi cha ‘Conference of the Parties’ unaohusisha wanachama wa UNFCCC-‘United Nation Framework Convention on Climate Change’, ambao ni mkataba wa kimataifa wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi uliopewa jukumu la kuwa chombo cha utekelezaji na usimamizi wa mkataba huo.

COP30 ni moja ya majukwaa muhimu zaidi duniani kwa majadiliano ya sera, mikakati na hatua za pamoja za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.