Mpanda FM

Mrindoko awapongeza waumini wa TAG Mpanda kwa kuliombea Taifa

28 October 2025, 9:45 am

Wachungaji wa TAG Mpanda wakiliombea Taifa. Picha na Anna Mhina

“Tunaliombea Taifa kwasababu ni agizo la Mungu”

Na Anna Mhina

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko amewapongeza waumini wa kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Bethel lililopo mtaa wa Kasimba kata ya Ilembo kwa kufanya maombi ya kuliombea Taifa na kuwasihi kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi la upigaji kura unaotarajiwa kufanyika October 29, 2025.

Mrindoko ametoa pongezi hizo alipokuwa mgeni rasmi kwenye ibada hiyo ya kuliombea Taifa katika kuelekea uchaguzi mkuu iliyofanyika jumapili October 26, 2025 na kuwataka waumini hao kuepuka vitendo vya uvunjifu wa amani na kuheshimu sheria za nchi.

Sauti ya mkuu wa mkoa

Awali akieleza sababu za kuliombea Taifa mchungaji kiongozi wa kanisa la TAG Bethel Evord Rugalinda ametaja sababu tano katika biblia ikiwemo Mungu kuahidi kuponya nchi endapo watu wake wataomba.

Sauti ya mchungaji

Maombi hayo ya kuliombea Taifa katika kuelekea uchaguzi mkuu yamefanyika ndani ya kanisa hilo na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya ya Mpanda na kamanda wa polisi mkoa.