Mpanda FM
Mpanda FM
22 October 2025, 1:16 pm

Picha ya pamoja wapili kutoka kulia ni mgombea ubunge jimbo la Mpanda kati Masanja Katambi. Picha na Betord Chove
” Kata ya Makanyagio ni kata ambayo miundombinu ipo hovyo”
Na Betord Chove
Mgombea wa udiwani wa Kata ya Makanyagio kupitia chama cha ukombozi wa Umma [CHAUMA] Rose Washa amesema ataboresha miundombinu ya barabara katika Kata hiyo.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa kuwanadi wagombea wa udiwani na ubunge wa kupitia chama hicho Washa amesema atakwenda kutengeneza miundombinu hiyo ambayo imekuwa mibovu katika kata hiyo na kuwataka wananchi kumpigia kura ili aweze kushinda na kuwaongoza kwa miaka mitano.
Aidha Washa ameanisha vipaumbele vingine akiwa madarakani ikiwemo suala la afya, pamoja na upatikanaji wa maji katika kata hiyo.
Akizungumza katika mkutano huo mgombea wa nafasi ya ubunge Masanja Musa Katambi amesema akipewa ridhaa atakwenda kuboresha sekta ya barabara, elimu, Afya ikiwemo kushughulika ana changamoto za kiuchumi ambazo zimekua zikiwakwamisha wananchi kupata huduma hizo.