Mpanda FM
Mpanda FM
22 October 2025, 12:45 pm

Afisa wa TAKUKURU Leonard Minja akizungumza na Mpanda radio. Picha na Anna Mhina
“Rushwa ikifumbiwa macho hupelekea jamii nzima kuathirika”
Na Samwel Mbugi
Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Katavi imeweka bayana athari zitokanazo na rushwa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.
Hayo yamesemwa na afisa wa TAKUKURU Leonard Minja akizungumza na Mpanda radio FM ambapo amesema kama itatokea wakachaguliwa wagombea wanaotokana na rushwa jamii haitaweza kupata maendeleo.
Minja ameongeza kuwa ili jamii iweze kupata maendeleo ya kweli inapaswa kuchagua viongozi wasiotokana na vitendo vya rushwa na kubadili mitazamo ya kutoa au kupokea rushwa ndio jambo linaweza kukuweka madarakani.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wameeleza kuwa rushwa inaweza kusababisha kupata kiongozi ambae sio sahihi na kushindwa kuwaletea maendeleo.
Kwa mujibu wa utafiti wa TAKUKURU wa mwaka 2024 kuhusu mianya ya rushwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaonyesha katika kila hatua za mchakato wa uchaguzi kunaviashiria na mianya ya rushwa kabla na baada ya uchaguzi.