Mpanda FM
Mpanda FM
20 October 2025, 5:01 pm

Waziri wa fedha Mwigulu Nchemba. Picha na mtandao
” Wengine wanasema serikali imeishiwa hela “
Na Restuta Nyondo
Serikali imesema kuwa Tanzania ina akiba ya fedha kiasi cha zaidi ya trilion 16 kiwango ambacho hakijawahi kufikiwa na hakuna nchi yeyote duniani yenye mtambo binafsi wa uchapishaji fedha.
Akizungumza wakati wa kampeni za mgombea uraisi wilayani Mpanda mkoa wa Katavi mgombea ubunge jimbo la Iramba magharibi kupitia chama cha Mapinduzi ambaye pia ni waziri wa fedha Mwigulu Nchemba amewataka wananchi kupuuza taarifa za upotoshaji zinazoenezwa kwenye mitandao ya kijamii.
Aidha Mwigulu amewataka wananchi kushiriki katika kuilinda amani na utulivu katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi October 29 na kutokubali kushawishiwa kuharibu amani ya Tanzania iliyolindwa kwa mda mrefu.
Hayo yamejiri baada ya taarifa mbalimbali zinazoenezwa kupitia mitandao ya kijamii zinazodai kuwa Tanzania imeishiwa fedha na kulazimika kuchapisha.