Mpanda FM
Mpanda FM
20 October 2025, 4:43 pm

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mpanda wa pili kutoka kulia akiwanadi wagombea wa jimbo hilo. Picha na Leah Kamala
“Ndugu zangu wa Kasokola kwenye kilimo Rais Samia amefanya kazi kubwa”
Na Leah Kamala
Mgombea Ubunge wa jimbo la mpanda mjini kupitia chama cha mapinduzi Haidary Hemedy Sumry amewataka wananchi kumwamini na kumpa ridhaa ya Kwenda bungeni kwa ajili ya kutekeleza mahitaji ya jamii.
Ameyasema hayo katika mkutano wa kampeni uliofanyika Kijiji cha sungamila kata ya kasokola na kuwahakikishia ataboresha huduma za afya ili kupunguza vifo vinavyotokea
Sumry ameongeza changamoto ya barabara inayowakabili wananchi wa Kasokola atahakikisha changamoto hiyo itakwenda kutamatika pamoja na kuwaahidi wakulima mbolea za ruzuku ili kuwawezesha kuzalisha kwa tija na kuongeza kipato.
Aidha Mgombea udiwani wa kata ya kasokola FiliberthIbumiamewaahidi mambo matatu wananchi wa kata ya Kasokola ambayo atakwenda kuyatekeleza ndani ya miaka mitano endapo watampa kura.
Nao baadhi ya wananchi wa kata ya Kasokola waliohudhuria mkutano huo wa kampeni wamewataka viongozi kutekeleza yale yote waliyoyaahidi ili kuwaletea maendeleo katika kata yao.
Vyama mbalimbali vinaendelea kuwanadi wagombea wao kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika October 29 mwaka huu.