Mpanda FM
Mpanda FM
18 October 2025, 5:49 pm

“kama watampa ridhaa ya kuendelea kuiongoza nchi atahakikisha mkoa wa Katavi unapata kipaumbele katika ujenzi wa barabara na madaraja ili kuunganisha mkoa huo na maeneo jirani ya ndani na nje ya nchi.”
Na Restuta Nyondo
Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi Dkt. Samia Suluhu Hassan ameahidi kuimarisha miundombinu ya usafiri na usafirishaji ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika uwanja wa Azimio halmashauri ya manispaa ya Mpanda amesema kama watampa ridhaa ya kuendelea kuiongoza nchi atahakikisha mkoa wa Katavi unapata kipaumbele katika ujenzi wa barabara na madaraja ili kuunganisha mkoa huo na maeneo jirani ya ndani na nje ya nchi.
Katika hatua nyingine Dkt. Samia amesema kuwa anatambua juu ya madai ya fidia ya wananchi waliopisha ujenzi wa barabara kwa muda mrefu na kuahidi kuwa ataielekeza wizara ya ujenzi kushughulikia changamoto hiyo.
Awali wakiomba kura ,wagombea Ubunge wa Jimbo la Mpanda mjini,Katavi,Nsimbo na Tanganyika wametaja changamoto ambazo watazipa kipaumbele kama vile maji,miundombinu na watumishi.
Chama cha Mapinduzi kimeendelea na kampeni za kunadi ilani ya chama hicho ikiwa zimesalia siku 11 kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika October 29 mwaka huu.