Mpanda FM

Wanachama 24 warudisha kadi za CHAUMA Mpanda

18 October 2025, 11:51 am

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mpanda katikati akipokea jezi za CHAUMA zilizorudishwa. Picha na Anna Mhina

“Wamerudisha kadi zao na jezi zao”

Na Anna Mhina

Wanachama 24 wa chama cha Ukomboza wa Umma ( CHAUMA) wa kata ya Kazima iliyopo manispaa ya Mpanda mkoani Katavi  wamerudisha kadi za uanachama kwa uongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Wanachama hao wamerudisha kadi hizo katika mkutano wa kampeni ya mgombea ubunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) jimbo la Mpanda kati uliofanyika katika viwanja vya Kwalakwacha uliopo kata ya Nsemulwa na kueleza sababu ya kuamua kurejesha kadi hizo ikiwa ni kutaka kushirikiana na kijana mwenzao ambaye wanaamini atawaletea maendeleo kwa haraka.

Sauti ya vijana

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Mpanda Joseph Iwamba amethibitisha kurudishwa kwa kadi hizo na kuwashukuru kwa kufanya maamuzi hayo.

Sauti ya mwenyekiti

Ikumbukwe kuwa ifikapo October 29, mwaka huu Tanzania inatarajia kufanya uchaguzi mkuu wa kuchagua madiwani, wabunge na Rais ambao watakaowaongoza kwa kipindi cha miaka mitano.