Mpanda FM

Masanja aahidi kutatua migogoro katika sekta ya madini Mpanda

16 October 2025, 4:07 pm

Viongozi wa CHAUMA wa pili kutoka kulia ni mgombea ubunge wa jimbo la Mpanda kati. Picha na Betord Chove.

” Naomba niwakikishie watu wa Dirifu ardhi hii ya uchimbaji ni mali yenu”

Na Betord Chove

Chama cha ukombozi wa umma wameendelea na kampeni kumnadi mgombea wa ubunge wa jimbo la Mpanda Kati katika kata ya Magamba mkoani Katavi.

Akizungumza katika mikutano  miwili iliyofanyika katika kijiji cha Dilifu na kijiji cha Mtakumbuka mgombea wa nafasi ya ubunge wa jimbo la Mpanda kati Massanja Musa Katambi amesema akichaguliwa atakwenda kutatua migororo iliyokuepo kwa muda mrefu na wawekezaji katika sekta ya uchimbaji wa madini katika Maeneo hayo.

Sauti ya Masanja

Aidha Masanja akizungumzia changamoto nyingine katika maeneo hayo amesema atakwenda kuboresha huduma za afya, elimu, maji pamoja na miundombinu ya barabara katika Vijiji hivyo viwili.

Sauti ya Masanja

Awali akizungumza mratibu wa kampeni wa chama hicho Almasi Mtije amewataka wananchi kumchagua mgombea wa chama hicho ili waweze kutatuliwa changamoto zilidumu kwa muda mrefu huku mmoja ya mwananchi wa kijiji cha mtakumbuka akimtaka Mgombea kushughulikia migororo ya wafugaji na wakulima akipata ridhaa.

Sauti ya mratibu wa kampeni

Vyama mbalimbali vinaendelea na mikutano ya kampeni kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika October 29 mwaka huu .