Mpanda FM

Sumry”nitatatua changamoto ya maji Mpanda”

16 October 2025, 3:50 pm

Mgombea ubunge jimbo la Mpanda kati akiwa kwenye kampeni zake. Picha na Anna Mhina

“Nitaboresha miundombinu ya barabara na maji”

Na Anna Mhina

Mgombea ubunge kupitia chama cha mapinduzi (CCM) jimbo la Mpanda kati Haidary Hemed Sumry amewaahidi wananchi wa kata ya uwanja wa ndege kuwaboreshea miundombinu ya barabara sambamba na kutatua changamoto upatikanaji wa maji katika eneo hilo.

Sumry ametoa ahadi hizo alipokuwa akifanya mkutano wa hadhara katika mtaa wa muunga mifupa uliopo kata ya uwanja wa ndege ikiwa ni muendelezo wa kampeni zake za kusaka kura kwa wananchi wa jimbo la Mpanda.

Sauti ya Sumry

Kwa upande wake mjumbe wa kamati ya siasa wilaya ya Mpanda Irene Temu amewaomba wananchi wa kata ya uwanja wa ndege kujitokeza kwa wingi siku ya 29/10/2025 kuwachagua viongozi watakaowaletea maendeleo katika kata yao.

Sauti ya mjumbe wa kamati ya siasa

Naye mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilaya ya Mpanda Joseph Iwamba ameeleza uzoefu aliokuwa nao mgombea ubunge wa chama hicho na kuwasihi wananchi kutofanya makosa ifikapo October 29.

Sauti ya mwenyekiti CCM Mpanda

Ikiwa vyama vya siasa vinaendelea na kampeni zake nchini kote, chama cha mapinduzi (CCM)  mkoa wa Katavi kinatarajia kumpokea mgombea urais kupitia chama hicho Dr. Samia Suluhu Hassan siku ya jumamosi October 18.