Mpanda FM
Mpanda FM
11 October 2025, 4:50 pm

Baadhi ya wafanyakazi wa NSSF Katavi. Picha na Restuta Nyondo
“Tunashukuru wajasiriamali tumefikiwa na sisi”
Na Restuta Nyondo
Zaidi ya wananchi 1000 waliojiariji katika shughuli ndogo ndogo za kiuchumi mkoani Katavi wamejiunga uanachana katika mfuko wa hifadhi ya jamii NSSF kwa mwaka.
Akizungmza na Mpanda radio fm wakati wa ufunguzi wa wiki ya huduma kwa wateja uliofanyika katika ofisi za Nssf meneja wa mkoa Jacob Sulle amesema mfuko huo umeanzisha mfumo wa hifadhi skimu kwaajili ya kusaidia kila mwananchi kujiwekea akiba na kunufaika na mafao kama ilivyo kwa wafanyakazi walioajiriwa.
Baadhi ya wananchama waliojiunga kupitia mfumo huo wamesema kuwa wanatarajia kunufaika zaidi na kuendelea kukuza biashara zao kupitia mikopo wanayoweza kupata katika mfuko huo.
Wiki ya huduma kwa wateja hufanyika kimataifa kila mwaka kuanzia 06 hadi 10 october ambapo kwa mwaka huu kwa upande wa Mfuko wa Nssf imebeba kauli mbiu isemayo Nssf Kidijitali tumeweza.