Mpanda FM
Mpanda FM
9 October 2025, 4:57 pm

Wafanyabiashara Katavi wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa TRA. Picha na Samwel Mbugi
” Ninyi ni watu mnaosababisha sisi tuendelee kuwepo”
Na Samwel Mbugi
Katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa katavi imewashukuru wafanyabiashara kwa kuendelea kulipa kodi na kufanikisha kuvuka lengo.
Akizungumza na baadhi ya wafanyabiashara kaimu meneja wa TRA Katavi Boniventure Kimaro ameeleza kuwa wamejipanga kuboresha huduma kwa wateja wao ili kurahisisha mifumo ya kodi.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Chemba ya wafanyabiashara mkoa wa Katavi Hassan Ally Dalla amewaomba watumishi wa mamlaka hiyo kuendelea kuwa na lugha nzuri katika utoaji wa huduma jambo hilo limepelekea wafanyabiashara kulipa kodi bila shuruti.
Naye mwenyekiti wa wafanyabiashara mkoa wa katavi Aman Mahella amewapongeza (TRA) mkoa wa Katavi kwa huduma ambazo wanazitoa kwani kipindi hiki kupitia dawati la uwezeshaji kumesaidia malalamiko mengi kutoka kwa wafanyabiashara.
Kauli mbiu ya wiki ya huduma kwa wateja mwaka huu wa 2025, ni HUDUMA BORA NI HAKI YAKO NA NI NGUZO YETU.