Mpanda FM

Kibonde aahidi kuboresha mazingira ya kujifunzia

9 October 2025, 3:19 pm

Mgombea urais Coaster Kibonde katikati akisalimiana na baadhi ya wanachama wa chama cha Makini. Picha na Samwel Mbugi

“Vipaombele vyetu vipo vitatu elimu, kilimo na afya”

Na Samwel Mbugi

Mgombea urais kupitia Chama cha Makini Coaster Kibonde ameendelea na kampeni zake katika Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi ambapo ameahidi kuboresha miundombinu ya usafiri, sekta ya elimu na afya endapo atachaguliwa kuwa rais.

Akizungumza na wananchi katika soko kuu la Mpanda, Kibonde amesema serikali yake italenga kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia ili kuhakikisha wananchi wanapata elimu bora na yenye tija kwa maendeleo ya taifa.

Sauti ya mgombea urais

Kwa upande wake mgombea ubunge jimbo la mpanda kati Martini Dues Tiho kupitia chama hicho amewahamasisha wananchi kujitokeza kwenda kumpigia kura ili aweze kuja kuwasaidi shughuli za maendeleo.

Sauti ya mgombea ubunge

Kwa sasa wagombea urais kutoka vyama mbalimbali wanaendelea na kampeni zao katika mikoa mbalimbali nchini wakieleza sera na kuomba ridhaa kwa wananchi kuelekea uchaguzi mkuu ujao.