Mpanda FM
Mpanda FM
3 October 2025, 3:11 pm

Mwenyekiti wa CHAUMA Katavi akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Mpanda mjini. Picha na Betord Chove
“Tunakwenda kuwatafutia mahali pa kufanya biashara zenu”
Na Betord Chove
Mgombea wa ubunge kupitia chama cha ukombozi wa umma {CHAUMA} Massanja Musa Katambi amesema atakwenda kurasimisha maeneo ya vituo vya boda boda ili waweze kumiliki maeneo hayo kwa uhalali wanavoendelea na biashara.
Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya soko la Ilembo kata ya Ilembo mkoani Katavi amesema kwa muda mrefu wasafirishaji hao wamekuwa wakisumbuliwa kwa kutokua na maeneo maalumu nay a kudumu ya biashara hiyo hivyo akipita nafasi ya ubunge atakwenda kumaliza changamoto hiyo.
Kwa upande wao baadhi ya vijana wanaofanya shughuli za usafirishaji wakizungumza mara baada ya kusikiliza sera za mkutano huo hususani urasimishaji wa maeneo yao wamepongeza kwa kutambuliwa kwa changamoto hiyo na wamesema kutatuliwa kwa changamoto hiyo kutaongeza ufanisi katika biashara zao.
Katika hatua nyingine Masanja amesema atakwenda kushughulikia sekta ya elimu, afya. Pamoja na kuhakikisha watu wenye uhitajimaalumu kama wenye ulemavu na wenye changamoto ya afya ya akili pamoja na wazee wanapata makazi na haki zote za msingi.