Mpanda FM
Mpanda FM
30 September 2025, 2:25 pm

Afisa kilimo kata ya Makanyagio Philemon Tesha. Picha na Anna Mhina
“Mimi nachukulia kilimo ni ile hatua ya mwisho ya kijana aliyefeli maisha”
Na Anna Mhina
Wakulima mkoani Katavi wametakiwa kuachana na kilimo cha mazoea na badala yake wajikite kulima kilimo chenye tija.
Akizungumza kwenye kipindi cha kilimo biashara cha Mpanda radio FM afisa kilimo wa kata ya Makanyagio Philemon Tesha amesema wananchi wengi hawalimi kilimo chenye tija hali inayopelekea kuonekana kilimo ni kama kazi ya watu masikini.
Fredy ni mkulima na mkazi wa kijiji cha Itenka A ambaye ameeleza faida mbalimbali alizozipata kwenye kilimo mbali na kupewa tuzo ya mkulima bora wa mkoa wa Katavi lakini pia amefanikiwa kununua usafiri kupitia kilimo.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa manispaa ya Mpanda wameeleza namna wanavyoichukulia kazi ya kilimo ikiwa ni pamoja na kuona ni kazi ya watu wasiosoma huku wakihitaji elimu itolewe ili kuwatoa katika mtazamo huo.