Mpanda FM

Mwanaume kutokuhudhuria kliniki madhara kwa mjamzito

29 September 2025, 12:44 pm

Omary Yusuph daktari hospital ya rufaa Katavi . Picha na Anna Mhina

“Anaposhiriki ananifanya nisione jambo la ujauzito kuwa ni gumu”

Na Anna Mhina

Baadhi ya wakazi wa mtaa wa Msasani uliopo kata ya Mpanda hotel manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameiomba serikali kutoa elimu juu ya umuhimu wa wanaume kuhudhuria kliniki pindi wake zao wanapokuwa wajawazito.

Wakizungumza na Mpanda radio FM baadhi ya wanawake wa mtaa huo wamesema wanapitia changamoto  ikiwemo kujifungua wakiwa dhaifu huku wanaume wakieleza sababu ya kutohudhuria kliniki ikiwemo utafutaji wa maisha na kuogopa kupima afya.

Sauti za wananchi

Nae mwenyekiti wa mtaa wa Msasani Juvenary Deus ameeleza namna atakavyotumia nafasi yake kama muwakilishi wa serikali pindi atakapobaini mwanaume hatoi ushirikiano kwa mkewe kipindi cha ujauzito ikiwemo kumpatia elimu.

Sauti ya mwenyekiti wa mtaa

Kwa upande wao baadhi ya viongozi wa kidini akiwemo sheikh mkuu wa mkoa wa Katavi Mashaka Nassor Kakurukuru na Askofu wa makanisa ya assemblies Anjelo Kachele wameeleza namna walivojipanga katika kutatua changamoto hiyo ikiwa ni pamoja na kuandaa semina maalumu kabla ya ndoa.

Sauti ya viongozi wa dini

Omary Yusuph ni daktari katika hospital ya rufaa Katavi kitengo cha magonjwa ya kina mama na wazazi ameeleza madhara atakayoyapata mama mjamzito ikiwa ni pamoja na kujifungua kwa upasuaji (operation), kuathirika kisaikolojia hali itakayopelekea kujifungua mtoto mwenye matatizo ya afya ya akili.

Sauti ya daktari