Mpanda FM
Mpanda FM
20 September 2025, 4:48 pm

Moja ya taa za barabarani katika halmashauri ya manispaa ya Mpanda. Picha na Sultan Kandulu
“Taa za barabarani kuwa mbovu zinaleta changamoto kwetu sisi watumiaji wa vyombo vya moto”
Na Sultan Kandulu
Watumiaji wa barabara mkoani Katavi wametakiwa kuchukua tahadhari nyakati za usiku wanapokuwa barabarani ili kuepukana na ajari kutokana na baadhi ya miuondombinu ya taa kutowaka wakati wa usiku.
Kwa upande wao baadhi ya watumiaji hao hasa madereva bajaji pamoja na pikipiki wamesema kuwa changamoto wanazokumbana nazo ni pamoja na ajari za barabarani wakati wa usiku.
Akizungumza kwa njia ya simu meneja wa TANROAD mkoa wa Katavi Mwandisi Martin Mwakabende ameeleza kuwa changamoto ya taa hizo kushindwa kuwaka ni vumbi lililoziba katika paneli za sola hizo na kusema kuwa marekebisho yameanza.
Aidha mwandisi Mwakabende amewataka wanufaika wa barabara nyakati za usiku kuongeza umakini pindi wanapokuwa barabarani kwa kipindi hiki ambacho wapo kwenye marekebisho.