Mpanda FM

Mwenge wa uhuru kutua Katavi Septemba 23, 2025

20 September 2025, 4:21 pm

Kulia juu ni mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko. Picha na Benny Gadau

“Mwenge wa uhuru unatarajiwa kutembelea miradi 46 yenye umbali wa 769”

Na Benny Gadau

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko amewataka wananchi kudumisha amani na utulivu kuelekea mapokezi ya mwenge tarehe 23/9/2025.

Mwanamvua amesema kuwa mwenge wa uhuru utapokelewa katika kijiji cha ifumbula kata ya mishamo halmashauri ya wilaya ya Tanganyika na kukimbizwa katika miradi ya maendeleo iliyopo katika wilaya hiyo.

Sauti ya mkuu wa mkoa

Aidha ameseme Mwenge wa Uhuru ukiwa Mkoani hapa utakimbizwa kwenye miradi mbalimbali yenye thamani ya zaidi ya bilioni kumi huku ukizunguka umbali wa zaidi ya kilomita 700 huku akiwataka wananchi kujitokeza barabara kuulaki mwenge huo.

Sauti ya mkuu wa mkoa

Kwa mwaka 2025 mwenge wa uhuru umebeba kauli mbiu isemayo UCHAGUZI MKUU 2025, JITOKEZE KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU 2025 KWA AMANI NA UTULIVU.