Mpanda FM

TRA Katavi yazindua dawati la uwezeshaji wa biashara

18 September 2025, 9:31 am

Viongozi mbalimbali katika picha ya pamoja, wapili kutoka kulia ni mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph. Picha na Benny Gadau

“Ushirikiano kati ya TRA na wafanyabiashara ni jambo la msingi sana”

Na Benny Gadau

Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imezindua dawati la uwezeshaji wa biashara kwa wafanyabiashara mkoani Katavi.

Akizungumza katika uzinduzi mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph amesema kuwa dawati hilo litakwenda kuwa msaada katika kutetea ukuaji wa kibiashara wa wananchi wa mkoa wa Katavi sambamba na kuweka mazingira Bora ya ulijali wa kodi kwa hiari.

Sauti ya mkuu wa wilaya

Akisoma risala kaimu meneja wa TRA mkoa  wa Katavi Benwad Peter  amewahakikisha wafanyabiasha kuwa mamlaka hiyo itaendelea kutoa ushirikiano ili kukuza uchumi wa mkoa na taifa kwa ujumla.

Sauti ya meneja TRA

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chemba ya wafanyabiashara mkoa wa Katavi Hassan Ally Dalla amewaomba watumishi wa mamlaka hiyo kutumia lugha nzuri katika utoaji wa huduma huku akiahidi kuendelea kutoa ushirikiano katika kuhakikisha wafanyabiasha wa mkoa hii wanatoa Kodi kwa hiari bila shuruti.

Sauti ya Dalla

Uzinduzi wa dawati hilo umeendana na kauli mbiu isemayo TRA KATAVI INASHIRIKISHA, INASIKILIZA NA INAWEZESHA.