Mpanda FM

MNEC Sampa azindua kampeni za CCM Nsimbo

16 September 2025, 3:56 pm

MNEC Gilbert Sampa kulia akimnadi mgombea ubunge jimbo la Nsimbo Anna Lupembe. Picha na Samwel Mbugi

“Tufanye kampeni za kistaarabu hakuna sababu za kutumia kejeli wala matusi”

Na Samwel Mbugi

Chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Katavi kimezindua kampeni jimbo la Nsimbo na kuahidi kuwatumikia wananchi kwa kuendeleza mambo mazuri ambayo yanafanywa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza mbele ya wananchi Mnec Gilbert Sampa ambae ni mgeni rasmi katika uzinduzi huo wa Kampeni amewataka wanachama wa chama hicho kufanya kampeni kistaarabu.

Sauti ya Mnec

Kwa upande waka Mgombea ubunge jimbo la Nsimbo Anna Richard Lupembe amesema endapo atachaguliwa kwa Mara nyingine ataenda kusimamia miradi na kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo la Nsimbo.

Sauti ya Lupembe

Ikumbukwe kuwa hivi karibuni mgombea mweza wa urais alifika mkoani Katavi na kuzindua kampeni hizo kimkoa na kunadi sera za chama hicho ambapo alieleza vipaumbele ni elimu, afya, kilimo na barabara.