Mpanda FM

CCM yazindua kampeni jimbo la Mpanda Mjini

16 September 2025, 1:31 pm

Picha ya baadhi wagombea nafasi mbalimbali za uongozi, wanne kutoka kulia ni mgombea ubunge jimbo la Mpanda mjini Haidary Sumry. Picha na Samwel Mbugi

“Yale ambayo tumeyaahidi 2020 tumeyatekeleza”

Na Samwel Mbugi

Chama cha mapinduzi CCM mkoa wa katavi kimezindua kampeni jimbo la Mpanda mjini na kuahidi kutekeleza ilani ya chama kwa kuwaletea wananchi maendeleo.

Akizungumza mbele ya wananchi Mnec Gilbert Sampa ambae alikuwa mgeni rasmi katika viwanja vya Sikonge manispaa ya Mpanda ambapo amesema mambo mengi yaliyoahidiwa 2020 yametekelezwa

Sauti ya Sampa

Kwa upande wake mgombea ubunge jimbo Mpanda mjini Haidary Sumry amesema kuwa endapo atachaguliwa ataenda kufanya kazi kwa kushirikiana na chama kwani ana uzoefu mkubwa katika utendaji kazi.

Sauti ya Sumry

Ikumbukwe kuwa siku za hivi karibuni mgombea mweza wa urais balozi Emmanuel Nchimbi alikuja mkoani Katavi kunadi Ilani ya Chama hicho Cha Mapinduzi (CCM)