Mpanda FM

Mgombea mwenza urais wa CCM kutua kesho Katavi

8 September 2025, 6:55 pm

Katibu wa siasa na uenezi CCM mkoa wa katavi Theonas Kinyonto. Picha na Samwel Mbugi

“Kutakuwa na mkutano mkubwa katika wilaya ya Mlele”

Na Samwel Mbugi

Chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Katavi kinatarajia kumpokea mgombea mweza wa Uraisi Dkt Balozi Emmanuel Nchimbi September 09,2025 kwa ajili ya kuja kunadi sera za chama.

Hayo yamesema na Katibu wa siasa na uenezi CCM mkoa wa katavi Theonas Kinyonto akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake ambapo amesema mkutano wake wa kwanza utafanyika kata ya majimoto na mkutano wa pili utakuwa viwanja wa maridadi kata ya Majengo.

Sauti ya Kinyonto

Pia kinyoto amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kufika katika viwanja hivyo kusikiliza kampeni za chama cha mapinduzi ili itakapofika siku ya uchaguzi wafanya maamuzi sahihi ya kuchagua kiongozi wanaemtaka.

Sauti ya Kinyonto

Hata hivyo amesema mikutano hiyo itaambatana na burudani kutoka kwa wasani mbalimbali wa mkoa wa katavi na inje ya mkoa wakiongozwa na Dogo Paten.