Mpanda FM

Wananchi Katavi walia na bei ya mitungi ya gesi

4 September 2025, 1:40 pm

Moja ya nishati safi ya kupikia. Picha na Hadija Paul

“Ni nzuri kwenye kupikia, changamoto ni bei”

Na Hadija Paul

Baadhi ya wananchi wa halmashauri ya manspaa ya Mpanda wameiomba serikali kutoa punguzo la bei ya mitungi ya gesi ili kurahisisha upatikanaji wa  nishafi safi ya kupikia kwa wananchi wa hali ya chini.

Wameimbia Mpanda radio FM kuwa bei ya mitungi ya gesi ni kubwa ukilinganisha na uwezo wao wa kiuchumi huku wakidai kushindwa pia kukidhi gharama za kujaza gesi inapokwisha ambapo bei kwasasa ya kununua ni shilingi 60,000 na kujaza mtungi ni kiasi cha shilingi 25,000  kwa mtungi mdogo.

Sauti za wananchi

Licha ya serikali kutoa ruzuku ya upatikanaji wa mitungi ya gesi kwa shilingi elfu kumi na tisa lakini ruzuku hiyo haikukidhi mahitaji kwani haikufika kwa wananchi wote wenye uhitaji.

Hivi karibuni Waziri mkuu Kasimu Majaliwa akiwa katika kampeni ya  uhamasishaji wa utumiaji wa nishati safi ya kupikia amewahamasisha watanzania kutumia nishati ili kuepuka adha ndogondogo kama vile magonjwa ya kifua kutokana na matumizi ya kuni na mkaa.

Sauti ya waziri mkuu

Serikali ipo kwenye mpango wa kuwezesha matumizi ya nishati safi ya kupikia kutoka asilimia 21 hadi asilimia 75  ifikapo mwaka 2030.