Mpanda FM
Mpanda FM
30 August 2025, 3:30 pm

Mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph. Picha na Anna Mhina
“Ninachoweza kusema ni kwamba magari yote yenye zaidi ya tani 10”
Na Sultani Kandulu
Mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusufu amewataka wafanyabiashara kushushia bidhaa zao katika eneo la maridadi ili kuepusha msongamano wa magari kwa maeneo ya soko na maeneo ya ndani ya mji.
Mkuu wa wilaya ya Mpanda Katavi Jamila Yusufu ametoa agizo hilo na kueleza kwamba magari yote kuanzia tani 10 yanatakiwa kushusha mizigo katika eneo la maridadi na kutaka agizo hilo litatekelezwa na yeyote atakayekiuka agizo atawajibika kulipa faini ya shillingi laki mbili.
Wakizungumza kwenye kikao cha kujadili changamoto baadhi ya wafanyabiashara wameeleza kuwa changamoto ya kushushia mizigo mbali na maeneo yao ya biashara inawaongezea gharama za usafirishaji mdogo kama bodaboda mikokoteni kupoteza muda, pamoja na kuongezeka kwa wizi na bidhaa zao.
Aidha meneja wa TARURA injinia Kahoza Joseph ameeleza kuwa kuna uwezekano wa kuharibu miundombinu ya barabara na mifereji ya maji andapo magari yenye uzito mkubwa yatashushia mizigo maeneo ya karibu.