Mpanda FM
Mpanda FM
28 August 2025, 6:57 pm

Moja ya makazi yanayotiririsha maji taka. Picha na Sultani Kandulu
“Kuna watoto wadogo wanaweza kuchezeachezea zile tope”
Na Sultani Kandulu
Wananchi wa manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wametakiwa kuacha tabia ya kutiririsha maji taka ili kuepukana na magonjwa ya mlipuko kama vile kipindupindu, tayphody na homa ya matunbo.
Akizungumza na Mpanda redio FM afisa afya manispaa ya Mpanda Erick Kisaka amesema utiririshaji ovyo wa maji taka ni hatari kwa afya za binadamu na kuongeza kuwa kwa yeyote atakayebainika hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake ikiwa ni pamoja na kushikwa faini ya shilingi elfu 50.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa manispaa ya Mpanda wameiomba serikali kutoa elimu juu ya madhara yatokanayo na maji taka ili kuweza kuwaepusha na changamoto mbalimbali.
Hata hivyo serikali inaendelea na kampeni ya kutoa elimu kwa wananchi pamoja na kufanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kudhibiti changamoto hiyo.