Mpanda FM

Lupembe ateuliwa rasmi kuwa mgombea ubunge jimbo la Nsimbo

28 August 2025, 3:30 am

Mgombea ubunge jimbo la Nsimbo Anna Lupembe na msimamizi wa uchaguzi jimbo la Nsimbo Julius Moshi. Picha na Restuta Nyondo.

“Kwa kuwa umekizi vigezo hivyo nakuteua kuwa mgombea ubunge jimbo la Nsimbo”

Na Restuta Nyondo

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Nsimbo kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM, mkoani Katavi Anna Richard Lupembe amerejesha fomu ya uteuzi wa kugombea ubunge  katika ofisi za msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Nsimbo.

Lupembe ameongozana na wanachama wa CCM pamoja wa wagombea udiwani wateule wa kata 12 zilizopo katika Jimbo hilo wamemsindikiza kurejesha fomu hiyo ambapo msimamizi wa Uchaguzi amesema kuwa ameteuliwa rasmi kuwa mgombea baada ya kukidhi vigezo.

Sauti ya msimamizi wa uchaguzi jimbo la Nsimbo

Aidha Lupembe amewashukuru  wananchi wa Jimbo la Nsimbo waliojitokeza kumsindikiza na kuwataka kushikamana na kuvunja  makundi na kupambania chama chao kupata ushindi.

Sauti ya Lupembe

Katika hatua nyingine msimamizi wa uchaguzi jimbo la Nsimbo Julius Zacharia Moshi amesema mpaka kufikia August 27 mchana wagombea wawili wa Ubunge kutoka chama cha ACT Wazalendo na Chama Cha Mapinduzi wamerejesha fomu na wamekidhi vigezo vya kugombea nafasi hiyo.

Sauti ya msimamizi wa uchaguzi jimbo la Nsimbo

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) Agosti 27 imefanya  uteuzi wa wagombea wa nafasi ya Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na wagombea wa Ubunge na Udiwani kote nchini.