Mpanda FM
Mpanda FM
25 August 2025, 6:48 pm

Jofrey Chaka mkaguzi wa polisi. Picha na Anna Mhina
“Mtembea kwa miguu anatakiwa atembee upande wake wa kulia”
Na Anna Mhina
Baadhi ya wananchi wa manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameiomba serikali kutoa elimu ya usalama barabarani kwa watembea kwa mguu ili kuwaepusha na ajali zinazoweza kuzuilika.
Wakizungumza na Mpanda radio FM baadhi ya watembea kwa mguu wameeleza kuwa hawana uelewa wa kutosha kuhusiana na matumizi sahihi ya barabara ikiwemo namna ya kutumia vivuko pamoja na upande sahihi wa kupita.
Jofrey Chaka ni mkaguzi wa polisi ambaye pia ni trafik operation ofisa mkoa wa Katavi ameeleza kuwa kisheria mtembea kwa mguu anapaswa kupita upande wa kulia mwa barabara ili kumsaidia kuona vyombo vya moto vinavokuja mbele yake na kuchukua tahadhari kwa haraka.
Aidha Chaka ameongeza kuwa mtembea kwa mguu anapaswa kufahamu matumizi ya vivuko ambavyo vipo kwenye mataa na kuhakikisha hapaswi kuvuka endapo taa yake husika haijamruhusu.
Hata hivyo kumekuwa na changamoto kwa baadhi ya madereva wa vyombo vya moto kutotii sheria za usalama barabarani hususani maeneo ya mataa na kwenye vivuko vya watembea kwa mguu (zebra) hali inayowapa wakati mgumu watumiaji wengine wa barabara.