Mpanda FM

Ofisi ya GIZ yazinduliwa Katavi

20 August 2025, 11:25 pm

Mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph( kulia) pamoja na Mkurugenzi wa shirika la GIZ (kushoto) wakikata utepe katika ufunguzi wa ofisi ya GIZ iliyopo Mpanda Plaza.picha na Anna Milanzi

ofisi hiyo itatumika na wadau mbalimbali katika kutekeleza mradi unaolenga kutatua changamoto mbalimbali hasa za uhifadhi wa maji

Na Anna Milanzi -Katavi
Shirika lisilo la kiserikali  kutoka nchini Ujerumani GIZ limezindua ofisi yake katika jengo la Mpanda Plaza manispaa ya Mpanda mkoani Katavi,uwepo wa ofisi hiyo mkoani  hapa inaongeza ufanisi zaidi katika utoaji wa elimu kwa jamii juu ya ulinzi wa miundombinu ya maji,viumbe hai na mazingira.

Ofisi hiyo pia itatumika kutekeleza mradi wa IKI KATUMA na kutatua changamoto mbalimbali za bonde la mto katuma ikiwemo uchukuaji maji kupita kiasi na changamoto zingine ambazo uleta  athari kwa viumbe hai.

Baadhi ya Wadau mbalimbali walioalikwa kushiriki uzindizi huo.picha na Anna Milanzi

Akielezea utendaji kazi wa shirika Mkurugenzi wa shirika hilo nchini Tanzania Anne Hahn amesema ufunguzi wa ofisi hiyo utaenda kusaidia usimamizi wa mradi wa IKI KATUMA wenye lengo la kulinda chanzo cha maji cha bonde dogo la mto katuma ambapo mradi huo utasaidia pia kulinda mazingira na kuondoa uharibifu na kusaidia kizazi cha sasa na baadae.

Sauti ya mkurugenzi GIZ nchini Tanzania akizungumza
Mkurugenzi wa shirika hilo nchini Tanzania Anne Hahn akizungumza .picha na Anna Milanzi

Mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph akitoa hotuba  kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amesema ufunguzi wa ofisi hiyo utasaidia utekelezaji wa mradi wa IKI KATUMA mradi ambao unalenga kufanikisha uendelevu wa bioanuwai katika bonde dogo la mto Katuma na kuleta maendeleo endelevu kwa wananchi na taifa kwa ujumla

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph akitoa hotuba
Mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph akitoa hotuba  .picha na Anna Milanzi

Nae mkurugenzi msaidizi katika idara za rasilimali za maji wizara ya maji Rosemary Robulisa amesema ofisi hiyo itatumika na wadau mbalimbali katika kutekeleza mradi unaolenga kutatua changamoto mbalimbali hasa za uhifadhi wa maji.

Sauti ya mkurugenzi msaidizi katika idara za rasilimali za maji wizara ya maji Rosemary Robulisa
mkurugenzi msaidizi katika idara za rasilimali za maji wizara ya maji Rosemary Robulisa .picha na Anna Milanzi

GIZ inafanya kazi nchini Tanzania kwa niaba ya Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ya Shirikisho la Ujerumani (BMZ) na washirika wengine wa kimataifa katika Kuhifadhi asili na maliasili, na viumbe hai,Afya, ulinzi wa kijamii na sera ya idadi ya watu, Jamii zenye amani na umoja, na utawala bora,Katika sekta ya bioanuwai, GIZ inaishauri Wizara ya Maliasili na Utalii Tanzania (MNRT) kutekeleza mkakati wa kitaifa wa kusimamia na kupunguza migogoro kati ya binadamu na wanyamapori.