Mpanda FM

Chaka: Tiini sheria za usalama barabarani

20 August 2025, 6:59 pm

Mkaguzi wa polisi Jofrey Chaka. Picha na Anna Mhina

“Hakikisheni vyombo vya usafiri vinakuwa bora”

Na Anna Mhina

Jeshi la polisi mkoani Katavi kupitia kitengo cha usalama barabarani limewataka watumiaji wa  barabara kutii sheria za usalama barabarani  ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika.

Akizungumza na Mpanda redio FM kwenye kipindi cha kumekucha Tanzania mkaguzi wa polisi Jofrey Chaka amesema mtumiaji wa barabara anapaswa kuhakikisha chombo cha moto kinakuwa bora kabla hakijaingia barabarani ikiwemo ubora wa mataili na honi.

Sauti ya afande Chaka

Katika hatua nyingine Chaka amewataka madereva bajaji kuacha tabia ya kusimama maeneo ambayo ni hatari kwa kisingizio cha kupakia abiria.

Sauti ya afande Chaka

Hata hivyo amewataka madereva wa pikipiki maarufu kama bodaboda kufuata sheria za usalama barabarani hasa wanapokua wakitumia barabara eneo la taa city Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi.