Mpanda FM
Mpanda FM
15 August 2025, 5:04 pm

Mkuu wa dawati jinsia na watoto Katavi Judith Mbukwa. Picha na Anna Mhina
“Tutengeneze ukaribu na watoto wetu kutawajengea usalama zaidi”
Na Roda Elias
Wazazi katika manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wametakiwa kuhakikisha wanasimamia ndoto za watoto ili ziweze kutimia.
Hayo yamesemwa na mkaguzi wa polisi Judith Mbukwa ambae pia ni mkuu wa dawati jinsia na watoto mkoa wa Katavi kuwa watoto ili wafikie malengo yao wanapaswa kulelewa katika maadili mema na malezi bora.
Mbukwa ameongeza kuwa mtoto hatakiwi kunyimwa adhabu anapokosea bali apatiwe adhabu ambayo inastahili kulingana na umri wake kwa lengo la kumuonya na endapo mzazi anapokiuka haki za mtoto serikali itachukua mkondo wake .
Kwa upande wao baadhi ya wazazi na walezi wa manispaa ya Mpanda wamesema kuwa kuwa karibu na watoto na kuwashirikisha mambo ya Mungu ndio kitu pekee kitakachowalinda watoto na kuwa na maadili mema.