Mpanda FM
Mpanda FM
12 August 2025, 1:38 pm

Moja ya mgawaha uliopo mtaa wa Mpanda hotal. Picha na Roda Elias
” Unakula chakula unakaa kidogo unaenda kununua flajiri”
Na Roda Elias
Baadhi ya walaji wa vyakula katika migahawa inayopatikana kata ya Mpanda hotel manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wamelalamikia suala la uchafu kwa mama lishe wa migahawa hiyo.
Wakizungumza na Mpanda Radio FM walaji hao wamesema kuwa wanakumbana na changamoto ya kula chakula kisicho safi hali inayowapelekea kuumwa kwa matumbo.
Kwa upande wao mama lishe wamekanusha malalamiko hayo huku wakiwaomba walaji pindi wanapoona mapungufu katika migahawa yao basi wawambie ukweli papo hapo.
Kwa upande wake afisa afya wa kata ya Mpanda hotel Mikidadi Ibrahim manispaa ya Mpanda mkoani katavi amesema kuwa zipo sheria zinazomtaka mama lishe kutoa huduma katika hali ya usafi na endapo atakaidi sheria hiyo atatozwa faini ama kufungiwa utoaji wa huduma ya chakula
Aidha Mikidadi ametoa wito kwa mama lishe hao kufuata sheria na taratibu ili kuepukana na faini zisizo za lazima.