Mpanda FM
Mpanda FM
8 August 2025, 1:16 pm

“mtoto huyo alitupwa katika moja ya chumba cha vyoo ambavyo vimesitishwa matumizi.“
Na Samwel Mbugi -Katavi
Mtoto mchanga anayekadiriwa kuwa na umri wa siku moja mweye jinsi ya kike ameokotwa kwenye choo cha shule ya msingi Kashato manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi.
Wananchi waliofika kushuhudia tukio hilo wamesema eneo hilo limekuwa likitumika vibaya na matukio kama hayo ambayo yamekuwa yakijirudia mara kwa mara ambapo wameiomba serikali kuweka uzio katika shule hiyo.
Mwenyekiti wa mtaa Buzogwe Lauresia Sanga amesema kuwa amepata tarifa kutoka kwa askari wa jeshi la ukoaji wakimtaka kufika eneo hilo wakidhani ni eneo ambalo analisimamia ili kufika kutoa ushirikiano.
Mwenyekiti wa mtaa wa Kigoma kata ya Makanyagio Athumani Lubwe amesema kuwa tukio hilo ni la tatu kutokea kwa miaka ya hivi karibuni hivyo ametoa rai kwa wadau mbalimbali kusaidia kuweka milango katika vyoo hivyo ili kusaidia kupunguza matukio kama hayo.
Hata hivyo jitihada za kumtafuta kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Katavi zinaendelea ili kutolea ufafanuzi wa tukio hilo ambalo linaonyesha kuwa ni tukio la tatu kwa hivi karibuni